FAIDA KUU ZA MLOZI (ALMONDS) KIAFYA

UTANGULIZI – MLOZI/ ALMONDS

Mlozi/ Almonds kwa lugha ya kigeni ni zao la jamii ya karanga. Linatumika karibu Duniani kote.

Mlozi/Almonds zina madini na virutubisho mbalimbali ambavyo huifanya kuwa na faida kubwa.

FAIDA ZA ALMONDS KIAFYA

  1. Husaidia Shinikizo la Damu (B.P). Mlozi/Almonds ina mafuta asilia yanayopunguza na kubalansi kiwango cha mafuta (cholestral) kilichozidi na kukuacha huru kwa kukuepushia Shinikizo la damu (B.P) na pia kwa mtu mwenye shinikizo la damu (B.P) hupunguza tatizo na kumfanya awe vizuri kwa kuwa in vitamini E
  2. Hupunguza Unene na Uzito. Kutokana na kuwepo kwa vyakula vyenye mafuta na sukari ambavyo huongeza uwezo wa kuzalisha mafuta (cholestrol) iliyombaya . Mlozi/ Almonds zina nyuzinyuzi, protein na mafuta asilia ambayo huthibiti na kupunguza mafuta ya ziada (yaliyozidi)
  3. Kuzuia kupata Saratani (Kansa). Mlozi/ Almonds zina virutubisho hasa vitamin E vinazozuia seli za kansa kuenea hii husaidia kwa wale wanaotumia mara kwa mara Mlozi(Almonds), Karanga, Korosho,
  4. Huondoa hatari ya mtu kupata Magonjwa ya Moyo. Mlozi/ Almonds zinaboresha Afya ya moyo kwa kuwa na vitamin E, pia kutokuwa na cholestrol hii hufanya Moyo kuwa imara.
  5. Huboresha Meno na Mifupa. Mlozi/Almonds zina vitamini na madini kama calcium, magnesium, manganese, copper, vitamin K, protein, and zinc, ambayo huimarisha mifupa na meno
  6. Ni nzuri kwa Wajawazito na Watoto. Zinavirutubisho na madini yanayohitajika na wajawazito na watoto. pia huongeza maziwa yenye afya nzuri.
  7. Huimarisha Kinga ya Mwili. Huongeza uwezo kunyonya au kufyonza madini na virutubisho. Pia huimarisha mmeng’enyo wa chakula hii hufanya mwili kuwa na kinga.
  8. Huimarisha Ubongo na uwezo wa kufikiri. Kutokana na kuwa uwezo wa riboflavin and L-carnitine ndio hufanya uwezo wa ubongo uwe mkubwa na kukuepusha na kupunguza mtindio wa ubongo.
  9. Huzuia tatizo la mmeng’enyo kama Constipation na Bawasiri. Husaidia kuongeza bakteria wazuri wanaoyeyusha chakula ili waweze kufanya mmeng’enyo uwe vizuri. Bila bakteria wa kuyeyusha chakula, chakula hakiwezi kuyeyuka vizuri.
  10. Huzuia Kisukari na Kusaidia wenye Kisukari. Kama tulivyoona, mlozi ni matajiri ya asidi ya mafuta, ambayo ina kazi muhimu sana kwa mwili, kwani husawazisha kiwango cha sukari kwenye damu yako na kudhibiti jinsi inavutwa na kutumiwa na mwili. Hii inamaanisha kuwa mlozi inaweza kukusaidia kudhibiti kiwango chako cha sukari ya damu na sukari yako. Kufanya tabia ya kula mlozi kunaweza kuzuia upinzani wa insulini, ambayo inaweza kuonekana wakati mwili uncharacteristicha kuguswa na insulini, ikiruhusu kiwango cha sukari kuongezeka sana. Faida zingine za matumizi ya mlozi ni kupunguza uzito usio na afya ya mwili na mafadhaiko ya oksidi.

VIRUTUBISHO NA MADINI KWENYE MLOZI/ ALMONDS

Mlozi/ Almonds hujivunia wasifu wa kuvutia wa virutubisho. Ombi 1-gramu (28-gramu) ya mlozi ina (1):

Nyuzi: gramu 3.5

Protini: 6 gr

Mafuta: gramu 14 (9 ambazo zimesimamiwa)

Vitamini E: 37% ya RDI

Manganese: 32% ya RDI

Magnesiamu: 20% ya RDI

Pia zina kiwango bora cha shaba, vitamini B2 (riboflavin) na fosforasi.

2 thoughts on “FAIDA KUU ZA MLOZI (ALMONDS) KIAFYA”

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.