Karibu Maisha Daily Org

Afya

Afya ndio nguzo kuu katika maisha. Bila kuwa na Afya Bora huwezi kuishi kwa Furaha na Amani. Maisha Daily tunakupa Elimu na Huduma ya Afya itakayokusaidia kuishi Kiafya.

Kilimo

Kilimo kina umuhimu mkubwa sana katika maisha kwa kutupatia Chakula na Malighafi mbalimbali katika uzalishaji wa bidhaa. Tulime Kiafya bila kutumia mbinu hatari.

Mazingira

Mazingira yanayotuzunguka ndio yanatufanya tuishi kiafya. Penda mazingira ili kupunguza hatari.Maisha Daily tunaelimisha na kuhamasisha utunzaji mzuri wa Mazingira.


Mikakati

Maisha Daily tuna mikakati mbalimbali kuimarisha Afya, Kilimo, na Mazingira ili kunusuru hatari ambazo zinaweza kujitokeza katika maisha yetu ya kila siku. Mikakati hiyo imlengwa ni kama ifuatavyo.

  • Afya: Kuhakisha jamii inaelimika kuhusu umuhimu wa Afya kwa kuwaelimisha kwa kutumia magazeti,mitandao, redio na hata televisheni. Pia katika midahalo mbalimbali inayohusu Afya. Kuacha kutumia vyakula na vinywaji vinavyoharibu Afya zetu, Kuwahimiza kutumia vyakula vyenye madini salama na asilia ili kuboresha Afya zao, Kufanya Mazoezi kwa kiwango kinacho shauliwa kiafya.
  • Kilimo: Kwa kuelimisha jamii mbinu bora za kilimo ili kufanikisha kutoa mazao bora yasiyo na hatari kiafya kama kuwaelimisha utumiaji wa mbolea zisizo hatarishi, kumfanya mkulima atambue madini yaliyopo kwenye ardhi yake na kutambua madini yaliyokosekana kwenye ardhi yake,
  • Mazingira: Kuifanya jamii ijue umuhimu wa mazingira katika maisha yetu. Pia kutatua changamoto za mazingira kwa kuondoa taka majumbani na mtaani pia kupunguza taka kwa kuzitumia katika uzalishaji, kuboresha mazingira na kuchimba mabwawa ya kuvunia maji ya mvua ili kunusuru mito yetu.

Ukuaji

Tunaendelea kuboresha huduma na kuendelea kutoa elimu kila mahali.

Tunaendelea kuongeza huduma na kuendelea kuelimisha jamii iwafikie jamii kwa upana.

Mafanikio

Tumebadilisha jamii kwa kuwapa Elimu ya Afya na wanajua jinsi ya kujali Afya zao, kuhusu Lishe Bora, mazoezi yaliyo salama, usingizi mzuri na vingine vingi. Pili ni kuhusu kilimo bora ambapo wakulima wengi tumekuwa tukiwaelimisha kuhusu kulima kiafya, matumizi ya vifaa na mbolea, kujali mazao na kutotumia mbinu mbaya zinazoweza kuwaathiri walaji na watumiaji wa mazao, kufanya kilimo kwa vitendo na kilimo biashara. Tatu ni tumeelimisha jamii kuhusu kutunza mazingira, kupanda miti, kutunza na kulinda vyanzo vya mito, kupunguza gesi ukaa.

Maisha Daily tunapenda kushirikiana na mashirika mengine, serikali, asasi, taasisi na sekta zozote zilizojikita katika Afya, Kilimo na Mazingira

Kuhusu sisi

Maisha Daily Org ni shirika (NGO) Inahusiana na kuelimisha, Kuhamasisha na kutoa huduma katika Afya, Kilimo na Mazingira

Mengi Kuhusu Maisha Daily

Mawasiliano

maishadaily@yahoo.com
+255 766797400

+255 763656541

Njia zingine za Kuwasiliana

Kufika

53302 Mlowo A104
Mbozi, Songwe Tz

Ramani na Miongozo

Kwa Huduma na Elimu ya Afya, Kilimo na Mazingira