SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER) – Aina, Chanzo, Dalili & Tiba

UTANGULIZI

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani inayotokea katika sehemu ya shingo ya uke ambapo sell za kansa hujiunda na kusababisha kizazi kupata madhara katika afya ya uzazi.
TAKWIMU

Saratani ya shingo ya kizazi inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi duniani. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya vifo hivi hutokea katika nchi zinazoendelea. Kwa Tanzania, wastani wa wanawake 6,241 huugua saratani hii kila mwaka, ambapo 4,355 kati yao hufa, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani (W.H.O) ya mwaka 2010

Saratani ya shingo ya kizazi ndio saratani ya kwanza kwa wanawake nchini Tanzania, na Saratani namba moja kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 44. Tanzania ina wanawake milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii. Kwa afrika mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya human papilloma virus ambavyo ndio visababishi vya ugonjwa huu.
AINA ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Kuna aina mbili za seli kwenye shingo ya kizazi (cervix) ambazo ni squamous cell na glandular calls, hivo saratani ambayo huanzia kwenye seli za squamous huitwa “squamous cell carcinoma” na saratani inayoanzia kwenye seli za glandular huitwa “adenocarcinoma”. Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba Saratani inapoanza huwa ni vigumu sana kuigundua kwani haioneshi dalili zozote, hivo unaweza usigundue mpaka pale saratani imefikia hatua mbaya Zaidi, pale ambapo dalili kama kutokwa na majimaji au maumivu wakati wa tendo la ndoa. Seli za kansa ya shingo ya kizazi hukua taratibu na huchukua miaka michache kwa seli za kawaida kubadilika kuwa seli za kansa, ndio maana inashauriwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua mapema.
CHANZO & SABABU ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu huwa na kisababishi kimoja au zaidi kinachojulikana ambacho huongeza hatari ya kuupata. Vifuatavyo ni visababishi vikuu:

  1. Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16)
  2. Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
  3. Maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus)
  4. Maambukizo ya magonjwa ya zinaa
  5. Umri zaidi ya miaka 30
  6. Upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI)
  7. Uvutaji wa sigara
  8. Kupata mimba katika umri mdogo
  9. Idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara
  10. Hali duni ya kiuchumi
  11. Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye mkewe alikufa kwa saratani ya shingo ya kizazi
  12. Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa
  13. Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia

Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo na kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja ni visababishi vinavyoongoza. Pia maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus), huchangia kwa kiasi kikubwa katika kusababisha ugonjwa huu.
DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.

  1. Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (vagina) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
  2. Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
  3. Maumivu wakati wa kujamiana.

Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo

  1. Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
  2. Kupungua kwa hamu ya kula
  3. Kupungua uzito
  4. Kuhisi uchovu
  5. Maumivu ya nyonga
  6. Maumivu kwenye mgongo
  7. Maumivu ya mguu
  8. Mguu mmoja kuvimba
  9. Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke
  10. Kuvunjika mifupa (bone fractures)
  11. Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.

MAKUNDI YA SARATANI YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi imegawanywa katika makundi kulingana na TNM ama FGO (Classification) kama ifuatavyo;
Stage I

Saratani iliyo kwenye chembechembe au seli za aina ya epithelium lakini haifiki kwenye nyama za ndani za shingo ya kizazi, Stage I – Saratani iliyopo kwenye shingo ya kizazi,
Stage II

Saratani iliyosambaa hadi kwenye tupu ya mwanamke sehemu ya juu kwa 2/3,
Stage III

Saratani iliyosambaa hadi kwenye ukuta wa nyonga na sehemu ya chini ya uke kwa 1/3, Hii inaleta madhara katika figo,
Stage IV

Saratani iliyosambaa hadi nje ya tupu ya mwanamke na pia husambaa hadi kwenye sehemu nyingine za mwili kama mapafu, figo, mifupa nk.
WATU GANI WAPO KWENYE HATARI KUBWA YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Kuna sababu zilizo ndani ya uwezo wako ambazo unaweza kuzifanyia kazi na kuunguza hatari ya kupata saratani hii, japo pia kuna njia ambazo ni vigumu kuepuka za ziko nje ya uwezo wetu kama vile uwepo wa saratani hii katika historia ya familia yako mfano kama mama ama dada yako aliwahi kupata saratani hii basi unaweza kuwa kwnye hatari kubwa nawe kupata. Makundi mengine ni kama

  • Wanawake kwenye umri kati ya miaka 20-50 wapo kwenye hatari Zaidi
  • Matumizi ya vidonge vya kupanga uzazi kwa mda mrefu.
  • Kuzorota kwa kinga ya mwili husabisha kuongzeka kwa athari ya virusi wa HPV wanaoletekeza kansa ya shingo ya kizazi.
  • Wanaopata ujauzito katika umri mdogo chini ya miaka 17 wapo kwenye hatari Zaidi ya kupata saratani hii.

MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Tiba ya saratani ya shingo ya kizazi hutegemea na hatua ya ugonjwa husika, na inahusisha

  • Kufanyiwa upasuaji na kuondoa mfuko wa mimba (uterus) na viungo vingine kama ovari na mirija ya uzazi
  • Matibabu kwa kutumia dawa kali(chemotherapy) ili kuongeza muda wa kuishi
  • Matibabu kwa njia ya mionzi ili kuua seli za saratani.
  • Kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu mara kwa mara.
  • Kupata chanjo dhidi ya virusi vya HPV kabla ya kuanza vitendo vya ngono.
  • Kupata elimu sahihi kuhusu ugonjwa huu.
  • Kujiepusha na mambo hatarishi yanayosababisha kuupata ugonjwa huu.
  • Ugunduzi wa mapema katika hatua za awali za ugonjwa huu na kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati.

MAMBO 10 UNAYOWEZA KUFANYA KUPUNGUZA HATARI YA KUUGUA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Usivute sigara wala kutumia tumbaku ya aina yoyote pia Hakikisha nyumbani kwako hamna moshi
  • Kuwa na mpenzi mmoja, Usichangie mapenzi na watu wengi
  • Kula chakula chenye afya hasa vyakula asilia
  • Kunyonyesha kunapunguza hatari kwa mama kuugua saratani
  • Hakikisha watoto wako wanapata chanjo dhidi ya hepatatis B na HPV
  • Epuka kuchomwa sana na miale ya jua, au tumia mafuta yanayo kukinga dhidi ya miale hiyo.
  • Epuka matumizi ya Dawa za uzazi wa mpango zenye madhara
  • Jishughulishe kuupa mwili mazoezi
  • Punguza unywaji wa pombe
  • Jitahidi kufanyiwa ukaguzi wa mapema kutambua uwepo wa saratani.

TIBA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Tiba ya saratani hii inategemea na kundi na aina ya saratani mgonjwa aliyonayo. Kuna Tiba ya kuchoma (cauterization), Tiba ya dawa (Chemotherapy),Tiba ya mionzi (radiation therapy), Tiba ya upasuaji (surgical treatment), Tiba Kwa kutumia Dawa Asilia (Herbal treatment).

Matatizo ya uzazi yanaweza kutibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za saratatani ya shingo ya kizazi na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.
DAWA

Tuna dawa ya kutibu ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda wa kuanzia miezi mitatu hadi miezi minne kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu, ukianza kutumia baada ya wiki mbili huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

Inajulikana kuwa watu wengi hawapendi dawa za mda mrefu wakati wana matatizo ya mda mrefu ambayo ni hatari, ni vigumu kupata dawa ya mda mfupi wakati una ugonjwa wa mda mrefu,

Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.

“Uamzi wako ndio kupona kwako”

MAWASILIANO

LOGO 1

MAISHA DAILY

S.L.P 66 MBOZI, SONGWE

maishadaily@yahoo.com

0766797400 /0763656541

2 thoughts on “SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER) – Aina, Chanzo, Dalili & Tiba”

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.