KILIMO BORA CHA BAMIA – OKRA

UTANGULIZI
Bamia ni zao la mbogamboga linalolimwa sana sehemu za joto, kwa lugha ya kigeni inaitwa Okra. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda yanayotokana na mmea. Zao hili linafaida sana kiafya, baadhi ya watu hutumia bamia kutengenezea mrenda. Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

ASILI YAKE
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines. Zao hili kwa sasa hulimwa maeneo mengi.

HALI YA HEWA
Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Andaa mbegu mapema kwa kawaida inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji kwenye bustani.

UPANDAJI
Mbegu za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani au shamba, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).Aidha kuotesha ili kurahisisha uotaji mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.
nafasi ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.

MBOLEA
Katika zao hili inashauriwa kutumia mbolea za asili (samadi na mboji) au takataka ili kurutubisha ardhi na kupata mavuno mengi. Ili kuzifanya bamia zako ziwe na mavuno mazuri basi hakikisha kama shamba lako lina rutuba basi panda kwa kutumia mbolea ya samadi na Kama halina rutuba basi pandia mbolea ya samadi au N.P.K (15-15-15)/(10-15-15) kiasi cha kilogram 50 – 100 na au wakati wa Mibamia kuweka maua tumia mbolea ya Urea Kilogram 25-30 kwa ekari au SA kilogram 50 kwa ekari.

UPALILIAJI & UNYEVU
Shamba la bamia inatakiwa lipaliliwe kwa kuondoa nyasi na liwe safi ili kudhibiti magonjwa na wadudu, unyevu unahitajika ili kuongeza mavuno.

MAGONJWA &WADUDU

MAGONJWA
Zao la bamia pia hushambuliwa sana na ukungu uitwao ubwiri unga, pia hushambuliwa sana na utitiri mwekundu na aphids. Kwa hiyo kila wiki dawa ya ukungu na sumu ya wadudu ipuliziwe kwenye mimea ili kuweza kukua katika ustawi uliobora zaidi, pia ni vyema kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa wataalamu wa kilimo.

WADUDU
Mosaic Virus– Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

UVUNAJI
•Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
•Kiasi cha kilo 8000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa vizuri.
•Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.

SOKO
Nchini Tanzania soko la bamia lipo. Inakadiriwa kuwa ifikapo kipindi cha masika bei ya bamia sokoni huwa juu. Hivyo mkulima atakayekuwa na mavuno ya bamia wakati wa masika anatarajiwa kuuza kwa bei ya juu kwa kuwa kipindi hicho zao hili huwa adimu katika soko.Ukilima eneo lenye ukubwa wa ekari 3 faida yake huwa kubwa zaidi kwani debe kidogoo cha lita 10 huwa 5000-6000 fedha za kitanzania.Ukilima kipindi cha kiangazi ambapo zao hilo huwa jingi sokoni hukadiriwa kidoo cha lita 20 huuzwa 3000-4000 fedha za kitanzania.

Contact/ Wasiliana nasi 

Phone (Simu): +255766797400 /+255673797408                                                    Email: daudilyela@yahoo.com

Maisha Daily LogoOur Services ( Huduma zetu): 

  1. Research( Utafiti),

  2. Drip Irrigation Installation (Ufungaji wa Umwagiliaji wa Matone)

  3. Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi),

  4. Business Plan ( Plani za Biashara),

  5. Profit Assessment ( Upimaji wa Faida)

  6. Agricultural Books (Vitabu vya kilimo)

 

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.