KILIMO BORA CHA NANASI

UTANGULIZI
Nanasi ni tunda ambalo mmea wake ni wa kitropiki ambao huzaa kwa kipindi, kitaalam Nanasi huitwa Ananas comosus,  Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam

ASILI YAKE
Asili ya nanasi inaaminika kuwa ni Brazil na Paraguay huko Amerika ya Kusini. Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini Tanzania maeneo ya Bagamoyo, Kibaha(Pwani), Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Hapa Tanzania, nanasi hulimwa zaidi maeneo ya Bagamoyo, Kibaha (Pwani), Tanga.

HALI YA HEWA
Nchini Tanzania Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 – 32, huwa haya stahimili baridi.

UDONGO
Kilimo cha nanasi chachu (pH) ya udongo inayofaa ni 5.5 hadi 6.0, na hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu na udongo wenye kichanga usiotuamisha maji ambao una rutuba ya kutosha. Ingawa nanasi huweza kustawi katika udongo wa aina yoyote ile, udongo wa mfinyanzi haufai kwa kilimo cha nanasi.unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Shamba la nanasi unaweza kulilima kwa sesa (flat-bed) au kwa matuta (furrows). Kwa sesa: chimba mashimo kwa nafasi ya sm.60 kati ya mistari, sm. 30 kati ya miche na sm. 80 kati ya kila mistari miwili. Weka mbolea kianzio katika kila shimo na upande, hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda. Weka tani 10 hadi 15 za mbolea ya kuku, weka pia viganja 2 vya mbolea ya zizi katika kila shimo.

UPANDAJI
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi.

MBOLEA
Kama utatumia mbolea za viwandani, weka mbolea ya NPK au DAP gramu 50 hadi 70 kwa kila mche wakati wa kupanda na . Weka tena gramu 85 kwa kila mche baada ya miezi 3 na pia miezi 3 baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU NA MAGONJWA
Kwa bahati nzuri Nanasi ni zao lisilosumbuliwa sana na wadudu ama magonjwa mara nyingi. Hii ni faida kubwa sna kwa wakulima wa nanasi! Hivyo endapo patatokea mashambulizi ya wadudu na magonjwa huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate,  Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug. Hakikisha unakagua shamba ili kuzuia wadudu kama wataonekana.Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides) kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Zao la Nanasi huanza kutoa maua miezi 12 hadi 15 baada ya kupanda kutegemeana na aina ya nanasi au maotea ya mbegu yaliyotumika, muda wa kupanda na joto la mahali husika. Kwa kawaida nanasi hukomaa miezi 5 baada ya kutoa maua, hivyo nanasi huchukua miezi 18 hadi 24 kukomaa/kuiva baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji  hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili. Katika kilimo cha nanasi, mimea ikitoa maua kwa nyakati tofauti tofauti itasababisha kuvuna kidogo kidogo na kwa muda mrefu. Kwa sababu hiyo ndio maana ni muhimu kupanda kwa wakati mmoja mbegu zenye umri na ukubwa sawa.

Contact/ Wasiliana nasi 

Phone (Simu): +255766797400 /+255673797408                                                    Email: daudilyela@yahoo.com

Maisha Daily LogoOur Services ( Huduma zetu): 

  1. Research( Utafiti),

  2. Drip Irrigation Installation (Ufungaji wa Umwagiliaji wa Matone)

  3. Project Proposal ( Mapendekezo ya Miradi),

  4. Business Plan ( Plani za Biashara),

  5. Profit Assessment ( Upimaji wa Faida)

  6. Agricultural Books (Vitabu vya kilimo)

 

6 thoughts on “KILIMO BORA CHA NANASI”

  1. MIMI NI MKULIMA WA NANASI KUTOKA BAGAMOYO, NAOMBA UNISAIDIE KWA UTUMIAJI WA MBOLEA AINA MOP ILI NIWEZE KUCHANGANYA NA AINA GANI MBOLEA ILI NANASI ZANGU NIWEZE KUVUNA MWEZI WA SITA MWAKANI. KWA SASA NANASI ZANGU ZINA MIEZI SABA

    Like

  2. Nimependa kilimo cha nanasi.
    Je ni kwanamna gani naweza kuanza kilimo hichi?
    Shamba ninalo na inaitajika niwe na kiasi gani cha pesa kwanzia kuandaa shamba mpaka mnunuzi ya mbegu na mbolea?

    Like

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.